← Rudi kwenye Nabii Adamu
Sehemu 1/5

Hadithi ya Adamu (1/5): Mwanadamu wa Kwanza

Hadithi ya kusisimua ya Adamu iliyoelezewa kwenye marejeleo kutoka kwa Vitabu Vitakatifu.
✍️ Aisha Stacey © 2008 IslamReligion.com 👁️ 22970 views 📅 09 Dis, 2021 🔗 Chanzo

Uislamu unatupatia maelezo ya kustaajabisha ya uumbwaji wa Adam. Tamaduni za Kikristo na Kiyahudi zinafanana sana na Kurani. Kitabu cha Mwanzo kinamuelezea kuwa Adam aliumbwa kutokana na "vumbi" na katika Talmud, Adam anaelezewa kuwa alifinyangwa kutoka kwa matope.

Na Mungu aliwaambia malaika: "Na pale Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa, wakasema: Utaweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua." (Kurani 2:30)

Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kutokana na kidonge cha udongo ulio na aina mbali mbali za udongo ardhini. Ulikuwa mwekundu, mweupe, hudhurungi, na mweusi; laini na nyumbufu, vile vile mgumu na wenye changarawe; kutoka milima na mabonde.

## Mchanga au Udongo?
Kila jina la udongo katika Kurani lilitumika katika hatua tofauti ya uumbaji wa Adam. Mwenyezi Mungu alifinyanga umbo la Adam kutokana na dutu hili. Kiwiliwili chake kiliachwa kukauka, na kuwa kama kile kinachofahamika kwenye Kurani kama udongo wenye sauti.

## Mwanadamu wa Kwanza Anathaminiwa
"Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotoka kwangu, basi muangukieni kwa kumtii." (Kurani 38:71-72)

Mungu akawaamrisha Malaika wamsujudie Adam. "Msujudieni Adamu. Basi wakasujudu isipokuwa Iblisi." (Kurani 7:11)

## Salamu ya Kwanza
Adam aliagizwa awasalimie Malaika kwa maneno Assalamu alaikum. Kuanzia siku hiyo salamu hizi zikawa za wale waliojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.

## Adam, aliye Mlinzi
"Na akamfundisha Adamu majina ya vitu vyote." (Kurani 2:31) Mungu alimpa Adam uwezo wa kutambua na kutaja majina ya kila kitu; alimfundisha lugha, hotuba na uwezo wa kuwasiliana.

💬 Maoni (0)

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuacha maoni!

Ingia ili kuacha maoni.