Baada ya kumaliza mambo yao East Blue, jamaa wa Straw Hat wakiongozwa na Luffy wanaanza safari ya ukweli sasa. Wanaelekea sehemu hatari sana ya bahari inayoitwa Grand Line — sehemu ambayo maharamia wakubwa wanatoka na mambo huwa magumu sana.
Ili kufika huko, wanapitia sehemu kama Reverse Mountain, mlima mkubwa ambapo bahari inapanda juu kama mto. Hapo wanaanza kuona kuwa safari yao haitakuwa rahisi hata kidogo.
Wakiwa njiani, wanatua sehemu inaitwa Whisky Peak. Mwanzoni watu wa hapo wanaonekana poa sana, wanawakaribisha na sherehe kubwa. Lakini baadaye inageuka kuwa kuna mpango wa siri unaohusisha kundi hatari linaloitwa Baroque Works.
Hapo ndipo mambo yanaanza kuchangamka:
-
Luffy bado yuko focused kuwa Mfalme wa Maharamia.
-
Zoro anaonyesha uwezo wake wa kupigana kama kawaida ⚔️
-
Nami, Usopp na Sanji wanajikuta kwenye matatizo mapya na maadui wapya.
Kwa kifupi, hii season inaonyesha mwanzo wa safari ngumu zaidi ya Straw Hats, wakikutana na maadui wakali, siri za dunia ya One Piece, na adventure kali zaidi kuliko East Blue. 🌊🔥
MAONI
Ingia ili uweze kutoa maoni.
Bado hakuna maoni.
— ANZA MAZUNGUMZO —Kuwa wa kwanza kusema kitu.