Mpangilio wa sahani Kwa Mgonjwa wa kisukari (Diabetic plate Guide) ni njia rahisi ya kumfundisha mgonjwa wa kisukari jinsi ya kupanga chakula kwenye sahani ili kudhibiti sukari ya damu.
-
Gawanya sahani katika sehemu 3
Nusu ya sahani (1/2) – Mboga
Weka mboga nyingi zisizo na wanga mwingi. Mfano: mchicha, kabichi, matembele, broccoli, spinach, biringanya.
Robo ya sahani (1/4) – Protini
Hii ni chakula kinachojenga mwili. Mfano: samaki, kuku, nyama isiyo na mafuta mengi, maharage, dengu, mayai.
Robo ya sahani (1/4) – Wanga (carbohydrates)
Weka kiasi kidogo cha wanga kama: ugali, wali, viazi, ndizi za kupika, mkate, wali wa kahawia.
-
Ongeza tunda kidogo pembeni
Chagua tunda moja kwa kiasi, mfano: apple, chungwa, papai kidogo, tikiti maji. Epuka kula matunda mengi kwa wakati mmoja. -
Tumia maji au vinywaji visivyo na sukari
Epuka soda, juice zenye sukari nyingi na chai yenye sukari nyingi. -
Epuka vyakula vya kukaanga sana
Chagua vyakula vilivyochemshwa. -
Kula kwa muda unaofanana kila siku
Hii husaidia kudhibiti sukari ya damu vizuri.
Mfano wa sahani kwa mazingira ya Tanzania
• Nusu sahani: mchicha na kabichi
• Robo sahani: samaki, kipande cha kuku (paja) au maharage
• Robo sahani: Ndizi, ugali au wali kidogo
• Tunda: kipande kidogo cha chungwa, Tufaa au Tango
Angalizo: maelezo haya ni mfano tu wa muongozo wa sahani kwa mgonjwa wa Kisukari kwenye wakati milo mikubwa miwili
Bado hakuna maoni.
Kuwa wa kwanza kusema kitu.