BONGOSOUL
Tupo Kwenye Kila Trend · Tanzania 🇹🇿
EST. 2024 🇹🇿
Nutrition & Diet

Je, Unafahamu Mgonjwa wa Kisukari anapaswa kula milo mingapi kwa siku?

Kwa mgonjwa wa kisukari, inashauriwa kula

🏥

Kwa mgonjwa wa kisukari, inashauriwa kula milo 3 mikuu na vitafunwa 1–2 kwa siku. Katika kila mlo, chagua kimojawapo kati ya vyakula vilivyotajwa.

  1. Kiamsha kinywa (Breakfast)
    Chagua kimojawapo kati ya:
  • Uji wa ulezi au mtama, Chai ya viungo na: Kipande cha mkate wa brown, Yai la kuchemsha, Mtindi usio na sukari, karanga n.k

 

  1. Chakula cha mchana (Lunch)
    Chagua kimojawapo kati ya wanga:
  • Ugali wa dona, Wali wa kahawia, Ndizi za kupika, Viazi vitamu

Kisha chagua kimojawapo kati ya protini:

  • Samaki, Kipande kidogo cha kuku, Maharage, Dengu

Na mboga:

  • Mchicha, Kabichi, Matembele, Kisamvu, Biringany, n.k
  1. Chakula cha jioni (Dinner)
    kama ilivyo chakula cha mchana isipokua punguza kiasi

 

  1. Vitafunwa (Snacks) kati ya milo
    Chagua kimojawapo kati ya: Tufaha, Tango, Karanga chache, biskuti zisizo na sukari, n.k
  2. N. B: Kuacha kula sio Tiba ya Kisukari
💬 MAONI 0

Bado hakuna maoni.
Kuwa wa kwanza kusema kitu.

— ANZA MAZUNGUMZO —